Pande CupNYUMBANIHABARIRATIBAWACHEZAJIPANDE CUP TVWADHAMINIKUTUHUSUTIMUTUZODUKA SAJILI TIMU
HADITHI YETU · KUTUHUSU

PANDE CUP
SI TU LIGI.
NI MFUMO WA
MTAA KUJIONA.

Pande Cup ni local football movement inayoweka structure, story, na digital thinking kwenye energy ya mpira wa mtaani.

Ilianzishwa na Festo Henry Msangawale baada ya kuona vijana wengi wanashinda mitaani bila kazi, bila direction, na bila kitu kinachowakusanya kwa purpose. Wazo likawa moja: kwa nini tusiunde league ambayo inaleta vijana pamoja, inaunganisha jamii, na inafanya mpira uwe mwanzo wa kitu kikubwa zaidi?

Soma hadithi
LIGI MOJA
UPENDO MMOJA
VUMBI MOJA

What Pande Cup Really Is

More than a cup, ni jukwaa la kuonyesha nguvu ya mtaa.

Pande Cup iliundwa kuonyesha kwamba football ya mtaani ikiwekwa kwenye mfumo sahihi inaweza kufanya zaidi ya kutoa bingwa. Inaweza kuunganisha vijana, kuamsha biashara ndogo, kujenga pride ya jamii, na kutoa image mpya ya grassroots football ya Tanzania.

In Practice

+League ya mtaani yenye structure, identity, na consistency
+Inakusanya vijana, mashabiki, na biashara ndogo za mtaa
+Inatumia media na digital storytelling kuongeza visibility ya grassroots football
+Imekua kutoka Kiomoni, Tanga hadi Goba, Dar es Salaam
01

Maana ya Pande

Huku mtaani, "Pande" si neno la kawaida. Ni ombi lenye uzito.

Kwenye muktadha wa mpira lina maana ya nipe nafasi. Kimitaani lina maana ya nipe fursa, nifungulie mlango, niamini. Ni sauti ya mtu anayesema: usiniache pembeni, niunganishe na nafasi yangu.

Hapo ndipo jina la Pande Cup lilipopata maana yake ya kweli. Halikuchaguliwa kwa sababu linasikika vizuri tu, bali kwa sababu linaeleza exactly kile ambacho vijana wengi wa mtaani wanahitaji: nafasi, connection, na mtu wa kuwaamini.

Kwa hiyo Pande Cup si jina la mashindano pekee. Ni kauli. Ni msimamo. Ni njia ya kusema kuwa kipaji cha mtaani hakiombi huruma, kinaomba tu kipewe pande yake.

02

Kwa Nini Ilianza

Wazo halikuanza na trophy. Lilianza na observation. Vijana wengi walikuwa na nguvu, ushindani, na passion, lakini walikuwa wanashinda mitaani bila direction ya pamoja.

Hapo ndipo ikaja idea ya kutumia mpira kama njia ya kuunganisha vijana na jamii, na kuipa energy ya mtaa mfumo unaoweza kuonekana na kuheshimika.

Background ya filmmaking, content creation, na digital tech ilinisaidia kuona jambo moja wazi: ndondo ikiwekewa structure na story sahihi, inaweza kuwa product ya culture yenye nguvu kuliko watu wengi wanavyodhani.

Hapo ndipo Pande Cup ikaanza kujengwa kama movement inayochukua football ya mtaani na kuipa identity, presentation, na heshima mpya.

03

Impact Halisi

Kilichotokea baada ya hapo hakikuishia kwenye scoreboard. Matchday zilianza kuwa sehemu ya mtaa kujiona upya.

Muundo wa Kweli

Ratiba, standards, na presentation vinavyoifanya ndondo ionekane serious na worth following.

Jamii Kwanza

Matchday inakuwa sehemu ya kukutana, kufanya biashara, na kuleta mtaa pamoja kuzunguka kitu chenye maana.

Storytelling Ya Kisasa

Football ikikutana na content na digital thinking, grassroots football inapata image inayoweza kuonekana, kukumbukwa, na kuuzwa.

Hapo ndipo tofauti ya Pande Cup ilipo. Sio mechi tu za wikiendi. Ni football inayobeba identity ya mtaa, energy ya jamii, na presentation inayofanya watu waione kama kitu cha kweli, si kitu cha kupita tu.

04

Zaidi ya Mpira

Kwenye Pande Cup, mpira ni mwanzo wa conversation kubwa zaidi. Vijana wanapata sehemu ya kuwekeza energy yao. Jamii inapata kitu cha kuzunguka kwa pride. Biashara ndogo zinapata watu. Mtaa unapata mood mpya.

"

Kila mechi haibebi matokeo tu. Inabeba umoja wa jamii.

Ndiyo maana Pande Cup inaweza kuonekana kama cup ya football, lakini kiuhalisia ni platform ya unity, visibility, na belonging.

05

Tunakoelekea

Pande Cup haikukusudiwa kubaki sehemu moja. Ilikusudiwa kuthibitisha idea kwanza, halafu kukua bila kupoteza roho yake ya mtaa.

Kiomoni

Mwanzo wa Harakati

Pande Cup ilianza kama jibu la moja kwa moja kwa vijana waliokuwa wanazunguka mitaani bila structure, bila excitement ya maana, na bila kitu kinachowakusanya.

Tanga

Ushahidi wa Model

Pale model ilipoanza kukaa sawa, ikathibitisha kuwa ndondo ikiandaliwa kwa heshima, jamii inaipokea, vijana wanaijenga, na mtaa unaiona kama kitu chake.

Dar es Salaam

Expansion Inayoonekana

Goba ni ushahidi kwamba Pande Cup si ya Kiomoni pekee. Ni idea inayoweza kusimama sehemu nyingine bila kupoteza roho yake.

Next

Vision ya Tanzania

Lengo si kuongeza mechi tu. Lengo ni kujenga ecosystem ya grassroots football inayounganisha talent, jamii, content, na opportunity kwa kiwango kikubwa zaidi.

Kutoka Kiomoni kwenda Tanga nzima.
Kutoka Tanga kwenda Dar es Salaam.
Kutoka hapo kwenda model ya Tanzania.

Vision ni kujenga football property ya grassroots inayoweza kusimama kwa nguvu ya community, culture, na presentation yake yenyewe. Si kwa kelele nyingi, bali kwa proof ya kila hatua.

JIUNGE NASI

KUWA SEHEMU
YA MOVEMENT.

Kama wewe ni brand, mdhamini, partner, creator, au mtu unayeamini kuwa grassroots football ya Tanzania inastahili kupewa image na hadhi mpya, Pande Cup ni sehemu ya kuijenga hiyo future kwa pamoja.

Built from the street, shaped for impact.

Pande Cup ni ushahidi kuwa mtaa ukipewa system, unaweza kutoa football experience yenye culture, biashara, na umoja wa kweli.

Kiomoni, Tanga
Goba, Dar es Salaam
+255 653 292 935
Wasiliana Nasi