Pande Cup
Sera ya Faragha
Imesasishwa: 18 Septemba 2026
Pande Cup ni bidhaa ya Msangawale Cinetech Solutions. Sera hii inaeleza taarifa tunazokusanya kupitia tovuti ya pandecup.co.tz na app ya Pande Cup ya Android, tunazitumia kwa nini, tunazihifadhi wapi, na haki zako.
Taarifa tunazokusanya
Unaposajili timu. Kocha au meneja anayejaza fomu anatupa:
- jina la timu, eneo lake, na picha ya jalada ya timu;
- jina, namba ya simu, barua pepe na picha ya kocha au meneja;
- majina, nafasi, namba za jezi na picha za wachezaji na wasimamizi wa timu.
Unapoagiza bidhaa dukani au kujiandikisha kusubiri nafasi, tunapokea jina lako, namba yako ya simu na ulichoagiza.
Unapozungumza na Gorilla Mwakere, tunapokea ujumbe unaoandika. Ukitumia sauti, tunapokea rekodi ya sauti yako ili tuigeuze kuwa maandishi.
Unapotumia tovuti au app, tunakusanya takwimu za matumizi: kurasa ulizofungua, aina ya kifaa na kivinjari, na eneo la jumla (nchi au mji). Hatukusanyi eneo lako kamili kupitia GPS.
Kwa nini tunazikusanya
- Kusajili timu, kuthibitisha wachezaji uwanjani (picha ndiyo kitambulisho), na kuonyesha vikosi, ratiba, matokeo na takwimu kwenye tovuti na app.
- Kuwasiliana na kocha au meneja kuhusu usajili, ada na mechi.
- Kushughulikia oda za duka.
- Kumwezesha Gorilla Mwakere kujibu maswali yako na kukumbuka mazungumzo yanayoendelea.
- Kuelewa jinsi tovuti na app zinavyotumika ili tuziboreshe, na kupima matangazo yetu.
Majina, picha, nafasi na takwimu za wachezaji zinaonekana hadharani kwenye kurasa za timu na wachezaji. Hilo ndilo lengo la ligi. Namba za simu na barua pepe haziwekwi hadharani.
Wanaopokea taarifa hizi
Hatuuzi taarifa zako. Tunatumia huduma hizi kuendesha Pande Cup:
- Supabase: kuhifadhi usajili, vikosi, mechi, oda na mazungumzo ya Gorilla.
- Cloudinary: kuhifadhi na kuonyesha picha.
- Vercel: kuendesha tovuti na app.
- Google (Gemini): kutengeneza majibu ya Gorilla Mwakere kutokana na ujumbe wako.
- Groq: kugeuza sauti yako kuwa maandishi unapozungumza na Gorilla.
- ElevenLabs: kugeuza majibu ya Gorilla kuwa sauti.
- PostHog na Vercel Analytics: takwimu za matumizi.
- Meta (Facebook) Pixel: kupima matangazo yetu kwenye Facebook na Instagram.
- WhatsApp: ukichagua kutuandikia au kukamilisha oda kupitia WhatsApp.
Huduma hizi zinaweza kuhifadhi taarifa nje ya Tanzania.
Wachezaji walio chini ya miaka 18
Pande Cup ina timu za vijana. Kocha au meneja anayesajili mchezaji aliye chini ya miaka 18 anathibitisha kuwa mzazi au mlezi wa mchezaji huyo amekubali jina na picha yake kutumika kama ilivyoelezwa hapa. Mzazi au mlezi anaweza kuomba taarifa za mtoto wake ziondolewe wakati wowote kupitia mawasiliano yaliyo hapa chini.
Tunazihifadhi kwa muda gani
Vikosi, matokeo na takwimu ni sehemu ya historia ya ligi na tunazihifadhi kwa muda wote ambao Pande Cup inaendelea. Namba za simu na barua pepe tunazihifadhi kwa muda timu inashiriki na kwa ajili ya kuwasiliana nayo misimu ijayo, isipokuwa ukiomba zifutwe.
Haki zako
Una haki ya kuomba kuona taarifa zako tunazohifadhi, kuzirekebisha, au kuziondoa. Kwa mchezaji, kuondoa taarifa kunamaanisha jina na picha yake kuondolewa kwenye kurasa za hadhara. Matokeo ya mechi yenyewe yanabaki kwa sababu ni ya timu zote mbili.
Tuandikie pandecup2023@gmail.com au piga/tuma WhatsApp +255 653 292 935. Tutakujibu ndani ya siku 30.
Mabadiliko ya sera hii
Tukibadilisha taarifa tunazokusanya au huduma tunazotumia, tutasasisha ukurasa huu na tarehe iliyo juu yake.
