Why It Matters
Tuzo Zinaongeza Uzito Kwenye Msimu
Hii page ipo kuweka wazi kuwa Season 2 haitaishia kwenye mechi tu. Itamalizika kwa recognition inayowafanya players, teams, na mashabiki wajue kuwa kila kitu kinahesabika.
Heshima Rasmi
Kila mshindi atatangazwa rasmi ndani ya ecosystem ya Pande Cup na kubeba title ya msimu mzima.
Visibility Ya Ukweli
Washindi na shortlist yao watapata spotlight kwenye website, socials, na recaps za msimu.
Tuzo Inafika Mtaani
Mshindi hapaswi kusafiri kufata heshima. Pande Cup inaifikisha mpaka kijiweni kwao.
Roadmap
Msimu Unavyojenga Awards
Badala ya kufungua kura mapema mno, tunaweka mfumo wa hatua kwa hatua ili awards zionekane credible na zije kwa uzito unaostahili.
Season 2 Kickoff
June 2026
Ligi inaanza na kila mechi inaanza kujenga kesi ya nani anastahili kutajwa mwisho wa msimu.
Tracking Ya Msimu
Wakati ligi inaendelea
Performances, moments, consistency, na impact vitafuatiliwa ili tuzo zisiwe za hisia pekee.
Shortlist Na Kura
Mwisho wa msimu
Baadhi ya tuzo zitachaguliwa na panel ya Pande Cup, nyingine zitaingia kwenye fan vote baada ya shortlist.
Delivery Ya Heshima
Baada ya matokeo
Washindi wanatangazwa, wanapigwa spotlight, na tuzo zinapelekwa moja kwa moja mtaani.
Categories
Tuzo Zinazoweza Kutikisa Mtaa
Categories hizi zinawekwa mapema ili teams na players wajue msimu huu unachezewa pointi za legacy, si matokeo pekee.
MVP wa Vumbini
Mchezaji aliyebeba mechi, tempo, na hofu ya wapinzani kwa consistency ya msimu mzima.
Ukuta wa Berlin
Kipa anayefanya timu yake iingie uwanjani ikiwa tayari inaamini haitafungwa kirahisi.
Master wa Pasi
Yule anayefanya wengine waonekane wakali kwa akili, timing, na final ball ya kibabe.
Bao la Kufuru
Bao ambalo litaendelea kuzungumziwa vijiweni hata baada ya mechi kuisha.
Kikosi cha Maangamizi
Timu iliyoonyesha utambulisho, ukomavu, na nguvu ya collective kuliko zote msimu mzima.
Kutoka Zero Hadi Hero
Player aliyepanda kiwango kwa namna ambayo kila mtu alilazimika kuanza kumhesabu upya.
Kinda la Kesho (U-21)
Kijana anayethibitisha kuwa msimu huu ni mwanzo wa jina kubwa linalokuja mbele.
Selection Logic
Sio Popularity Contest Tu
Hizi awards zinatakiwa zijenge credibility ya Pande Cup, kwa hiyo mfumo wake una balance kati ya football truth na fan excitement.
Sio kura tupu
Tuzo zote hazitategemea popularity pekee. Kuna categories zitahitaji ushahidi wa performance na impact ya msimu.
Hybrid model
Zile tuzo zinazohitaji heat ya mashabiki zitapata shortlist kwanza, halafu fan vote itaingia kwenye hatua ya mwisho.
Legacy ya msimu
Lengo si tu kumpa mtu zawadi. Lengo ni kufanya kila mechi ya Season 2 ijenge legacy ya mwisho wa msimu.
Notify Me
Shtuka Tuzo Zikianza
Dondosha namba yako sasa. Tutakushtua shortlist, nominations, au fan vote ikikaribia kufunguliwa baada ya msimu kuchanganya.
Pande Cup Awards kwa sasa ni preview ya mkakati wa mwisho wa msimu. Season 2 ikianza June 2026, kila performance linaanza kujenga nafasi ya kutajwa, kushortlistiwa, au kupewa heshima ya mwisho wa msimu.
